Kama wewe ni Vlogger, Bloger, mtangazaji au Muandishi wa Habari na una lengo la kuanza kutumia mtandao wa YouTube ili uweze kujiingizia kipato basi kuna vigezo vipya vimeongezwa.
Kwa sasa Mtandao huo utahitaji mtumiaji awe amefikisha masaa 4,000 yaani dakika 240,000 ya kutazamwa kwenye akaunti yako kwa miezi 12 iliyopita ili uweze kuiwezesha akaunti yake ya YouTube kulipa ‘Monetization’ .
Licha ya kigezo hicho, pia vigezo vya awali vya kuwa na angalau Subscribers 1,000 na watazamaji (views) 10,000 bado vitaendelea kutumika kama vigezo vya msingi vya kuwezesha akaunti yako kuanza kulipa ‘Monetization’ .
Masharti hayo yameanza kufanya kazi mwezi wa Februari kwa nchi ya Marekani na kwa nchi nyingine yameanza kufanya kazi mwezi Marchi ambapo masharti hayo hayatahusisha akaunti ambazo tayari zilianza kulipwa kwa masharti ya awali. Hii ni kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Paul Muret .
Post A Comment: