Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wa Mashindano, Hussein Nyika, umesema kuwa umekata rufaa TFF kulalamikia mchezaji mmoja wa Mbeya City kuzidi Uwanjani.

Nyika ameeleza kuwa wametuma malalamiko hayo kufuatia mchezaji wa Mbeya City kuonekana Uwanjani wakiwa 11 badala ya 10 wakati mmoja wao alikuwa ameshapewa kadi nyekundu.

Yanga wamefikia hatua ya kufanya hivyo baada ya beki wa Mbeya City, Ramadhan Malima kupewa kadi nyekundu, na kisha baadaye kuonekana tena Uwanjani wakati zikiwa zimebakia dakika takribani 6 mchezo kumalizika.

Wakati mechi hiyo ikielekea mwisho, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alionekana akibishana na Kamisaa wa mchezo huo, kuhoji kwanini Mbeya City wapo 11 badala ya 10.

Nsanjigwa alionekana akiwa amepandisha munkari akitaka kujua kipi kilichosababisha mpaka aendelee kusalia Uwanjani wakati kanuni haziruhusu.

Mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, ilimalizika kwa sare ya 1-1, Yanga wakifunga kupitia Rafael Daud na Mbeya City kupitia Iddy Naddo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: