Mabingwa wa Soka Tanzania, Yanga wako njiani kurejea jijini Dar es Salaam.
Yanga na Simba, zinakutana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara na zote ziliweka kambi mkoani Morogoro.
Jana, vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba walirejea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo wa keshokutwa.
“Yanga wameondoka huku muda si mrefu wakirejea Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho,” kilieleza chanzo.
Post A Comment: