Yanga SC imefanikiwa kutinga hatua ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu baada ya kuitoa nje ya mashindano hayo timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia hapo juzi kwa jumla ya mabao 2 -1.
Yanga SC ikiwa haina uzoefu wa kutosha kwenye hatua hiyo itakutana na timu nane ambazo nazo zinashiriki kwa mara ya kwanza zikiwemo mbili kutoka Afrika Mashariki.
Viongozi wa CAF wanatarajia kukutana hapo kesho makao makuu ya Shirikisho hilo Cairo, Misri kwaajili ya ratiba ya michuano hiyo.
Timu kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki zilipata nafasi ya kutinga hatua hiyo ni, Yanga SC, Gor Mahia ya Kenya na Rayon Sports ya Rwanda.
Miongoni mwa timu nyinge zilizopata nafasi ya kushiriki kwa mara ya kwanza ni El Masry ya Misri, Wiliamsville kutoka Ivory Cost, Aduana ya nchini Ghana na RS Berkane.
Jumla ya timu zote zilizofanikiwa kuingia hatua ya makundi ni AS Vita (DR Congo), USM Alger (Algeria), El Masry (Egypt), Raja Club Athletic (Morocco), CARA (Congo), El Hilal (Sudan), Gor Mahia (Kenya), UD Songo (Mozambique), Enyimba (Nigeria), Aduana (Ghana), Young Africans (Tanzania), RS Berkane (Morocco), Williamsville (cote d’Ivoire), Djoliba (Mali), Rayon Sports (Rwanda).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: