Wema
Sepetu amempiga dongo Mange Kimambi kufuatia maandamano aliyokuwa
akiyahamasisha kupitia mitandao ya kijamii akiwataka Watanzania
waandamane kutokufanikiwa.
Mange
alikuwa akiwashawishi Watanzania kuandamana leo katika maadhimisho wa
miaka 54 ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya kupinga baadhi ya
mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano, lakini hata hivyo,
maandamano hayo hayajafanyika katika kiwango kilichokuwa kikidhaniwa.
Watu
wengi leo walikaa majumbani mwao wakihofia kutoka nje kutokana na
polisi kutishia kuwashughulikia wale wote watakaoandamana, hali
iliyopelekea baadhi ya watu kukatisha shughuli zao.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram Wema amesema kuwa alisitisha safari yake ya
kwenda Arusha kutokana na hofu kuwa kungekuwa na maandaamano, kumbe
hakuna kitu chochote.
“Watu
Tukajua Kuna Maandamano mpaka Safari tukazihairisha… Kumbe hamna kitu…
Ila utani tuweke pembeni wengi wetu tulishtushwa… But one thing y’all
have to understand is Wa Moja Wa Moja tu… Aliepewa kapewa… And Kamwe
huwezi shindana na POWER.”
Aliendelea
kusema, “ARUSHA… Tunaomba Radhi… We had to Cancel our Trip sababu ya
Haya Mambo ya Uongo na Kweli… But Tunakuja Soon tutawajulisha wapendwa
wetu.”
Licha
ya kuwa Wema hakumtaja Mange katika ‘post’ yake, lakini ni dhahiri kuwa
dongo hili limeelekezwa kwa Mange kwani ndiye alikuwa mhamasishaji mkuu
wa maandamano haya ambayo Wema amesema ni ya uongo.
A
Post A Comment: