WAZIRI Wa Afya Maendeleo ya Jamiii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka matangazo katika vituo vya afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za upimaji na matibu ya Malaria ni bure na wananchi na hawatakiwi kulipia kwakuwa kuna wafadhili wanaogharamia tiba hizo.
Maagizo hayo aliyatoa juzi Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga wakati akizindua ugawaji wa endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu, kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa ushirikiano wa Serikili ya Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Mpango huu unaendeshawa na shirika la John Hopkins na Vectors chini ya ufadhaili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria.
Post A Comment: