WAZIRI
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Profesa Makame Mbarawa (MB)
jana tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya
Shirika la Posta Tanzania.
Mhe.
Profesa Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania
kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za
Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi
ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dr. Haruni
Kondo.
Katika
ziara hiyo Mhe. Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya
kielektronik na namna ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo
mbalimbali ili kusimamia utendaji kwa ukaribu.
Mhe.
Waziri Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki,
Idara ya Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo udhibiti wa
gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika yanayosafiri kati ya
Dar es salaam na mikoani.
Katika
ziara hiyo Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia
utendaji kazi na kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya
kielektroniki na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali
ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Mhe.
Waziri alitoa msisitizo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi
na kukuza tija kwa kila Idara ndani ya Shirka la Posta. Waziri
amemwaagiza Kaimu Postamasta Mkuu Hassan Mwang’ombe kufuatilia utendaji
wa kila idara na kupata taarifa za mara kwa mara ili kuimarisha utendaji
wa shirika.
Mwenyekiti
wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta alimshukuru Waziri Mhe.
Mbarawa kwa kutembelea Shirika la Posta na kuahidi kuwa maagizo yote na
maelekezo aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu ili kuleta tija na Ufanisi
zaidi.
Post A Comment: