WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi
kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi
wanaowaongoza ni wa vyama vyote.
Pia
amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana
ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia
ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.
Ameyasema
hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya
Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri
Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.
“Viongozi
wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo
wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama
vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.”
Waziri
Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na
viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia
amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya
nyenzo zinazochochea maendeleo.
Akijibu
ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za
kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi
kuwa Serikali itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu
yao kama ilivyokusudiwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Post A Comment: