Na Mahmoud Ahmad Dodoma
Serikali
imewataka watumishi wa umma kujitathmini katika utendaji wao wa
kuwahudumia wananchi wanyonge kwa matendo yao kama yanalingana na
mwenendo wa mh. raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkta John Pombe
Magufuli katika kuwahudumia wananchi wanyonge.
Kauli
hiyo imetolewa jana na waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo
wakati akizindua mnara wa magufuli kwenye chuo cha serkali za Mitaa
Hombolo ambapo amewataka kuhakikisha wanajitathmini katika matendo yao
ya kila siku katika kuwahudumia wananchi.
Amesema
kuwa wanafunzi wanaosoma hapo wanatakiwa kuanza kujitahmini kimatendo
kama wana uwezo na moyo wa kuitumikia jamii kwani wajibu wao wa kwanza
kujua wanaenda kushughulikia kero za jamii.
"Nawasihi
vijana kuanza kujiangalia na kujitathini kiutendaji wao kama wanafanana
matendo yao na mh.rais ili kuweza kuisaida jamii kwani wajibu wa msingi
ni kufanyakazi kwa bidiii" alisisitiza Jaffo.
Aidha
kwa upande wake mwenyekiti wa chuo hicho Suleiman Ngware wazo la
kujenga mnara huo utakaoitwa (MAGUFULI SQUERE) Lilibuniwa na bodi ya
chuo lieweka mbele maslahi mapana ya utendaji wa umma katika kutoa
huduma bora bila kuangalia wala kubagua wananchi kwa hali zao.
Amesema
kuwa sehemu hiyo ni sehemu ya kuanza kujitathmini kwa matendo yetu ya
kila siku katika kuhudumia wananchi na wanafunzi watakao toka hapa wana
wajibu wakuwa mabalozi wazuri katika utumishi wao ili taifa lifikie
malengo kusudiwa.
Nae
Mkuu wa Chuo hicho Dkta Mpamila Madale amesema kuwa kila tarehe kumi
nane chuoni hapo watakaa eneo la mnara huo kuangalia suala zima la
utendaji na kujitathmini kama wamefikia malengo katika utendaji wao wa
kila siku.
Amesema
kuwa mnara huo lengo lake ni kuwa chemu chemu ya utendaji unaofanana na
mh.rais kufikia maengo ya kutoa watumishi wenye uzalendo na nchi yao
ili kila mtanzania ajue wajibu wake kwa nchi yake.
Post A Comment: