Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia watuhumiwa 49 waliokamatwa katika matukio matatu tofauti ikiwemo wahamiaji haramu 23, wezi wa pikipiki 13 na uchochezi kwa njia ya mitandao 13.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kuwa Jeshi hilo linawashikilia wahamiaji 23 kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria. Ameeleza watu hao walikuwa kijijini Chikongola Wilaya ya Mtwara ambapo askari wa doria walipewa taarifa na raia wema na kufika eneo hilo.

Kamanda ameeleza kuwa mtandao wa wezi wa pikipiki ulikuwa na kambi katika kijiji cha Chikongo wilayani Tandahimba ambapo walikuwa wakiiba pikipiki na kwenda kuziuza kwa tajari mmoja ambaye huzisafirisha kuziuza nchini Msumbiji.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi Mtwara linawashikilia wanafunzi 9 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara na Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba halmashauri ya mji wa Nanyamba kwa kosa la kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo ‘Watsapp’ na Telegram’ kuhamasisha maandamano.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: