Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha
kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue,
Posta.
Watu hao wamekamatwa baada ya Jeshi la Polisi kuonya kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la kutoandamana kama walivyoagiza.
Watu
hao walikuwa wakiandamana kufuatia maandamano yaliyohamasishwa kupitia
mitandao ya kijamii yeye lengo la kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa
na serikali.
Mbali
na watu hao, baadhi ya maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam leo
yamekuwa na watu wachache sana tofauti na siku nyingine za mapumziko,
ambapo watu wengi wamekuwa na hofu ya kutoka, kutokana na tetesi za
kuwapo kwa maandamano.
Post A Comment: