Watoto wa kike 5,913 wamepata ujauzito katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu mkoani Tabora.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati anafungua semina ya siku moja ya Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi ya Mkoa huo.
Alisema takwimu hizo zinasikitisha na zinaoonesha kuwa bado kuna tatizo kubwa la watu wazima kukatisha ndoto za watoto wa kike mkoani humo.
Mwanri alisema Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ndio inaoongoza kwa watoto 1438 , ikufuatiwa na Igunga 995, Kaliua ambayo ina watoto 894 , Sikonge 743, Uyui 640 , Urambo 630, Manispaa ya Tabora 530 na Nzega Mji 49.
Alisema vitendo hivyo sio vinarudisha nyuma maendeleo ya watoto bali vinawaweka katika hatari ya kupata saratani ya mlango wa kizazi kwa kushiriki ngono katika umri mdogo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: