Zaidi ya Watoto wa kike 20,000 wenye umri wa miaka 14 watapatiwa chanjo ya saratani ya shingo ya uzazi mkoani Arusha katika jumla vituo vya afya 372 pamoja na shule zitakazoanisha kutumika katika utoaji wa chanjo hiyo.
Mratibu wa Chanjo mkoa wa Arusha Aziz Sheshe amesema kuwa chanjo hiyo itawakinga watoto kike na ugonjwa huo ambao husababisha maumivu makali na hata kupelekea vifo vya watoto.
Azizi amesema kuwa tayari vituo 292 viko tayari kwa kutoa huduma hiyo hivyo amewataka watoto wenye umri huo kujitokeza katika vituo hivyo ili kupata huduma bora ya chanjo inayotolewa na serikali.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema kuwa ni vyema jamii ikaondokana na mila potofu ambazo hujitokeza kwani chanjo hiyo ni salama na itakoa maisha ya watoto wa kike wanaopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa saratanii ya shingo ya uzazi na matiti husababisha karibu asilimia 50% ya vifo vyote.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Timoth Wonanji amesema kuwa chanjo hiyo ni juhudi za serikali na wa maendeleo katika kupambana na saratani ya mlango wa uzazi ambayo inakua kwa kasi hivyo juhudi hizo zitasaidia kupunguza ama kutokomeza ugonjwa huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo na Naibu Meya wa Jiji la Arusha Viola Lazaro wamesema kuwa chanjo hiyo ni mkombozi wa watoto wa kike katika taifa la Tanzania hivyo amewataka Watoto wa kike kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata kinga inayotokana na chanjo hiyo.
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia;
Post A Comment: