Wafanyakazi wote mjini Morogoro wameombwa kesho Mei Mosi wajitokeze kwa wingi kwenye maandamano yatakayoambatana na sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.
Wito huo umetolewa jana Jumapili Aprili 29, 2018 na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Mashambani (TPAWU), Nocholaus Ngowi wakati akizungumzia maandalizi ya sherehe za Mei Mosi.
Ngowi amewata wafanyakazi wote mjini humo wajitokeze kuandamana ili waweze kuweka bayana changamoto zinazo wakabili.
Kwa upande mwingine, Mratibu wa maandalizi ya sherehe hizo mkoani Morogoro, Mgassa Chimola amewaomba waajiri kuwaruhusu wafanyakazi wao kuhudhuria kwenye sherehe za maadhimisho hayo ili kujua haki na wajibu wao.
Chimola amesema maadhimisho hayo yataanza kwa maandamano katika ofisi za TUICO na baadaye kuelekea katika Uwanja wa mpira wa Jamhuri na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe S. Kebwe.
Sikukuu ya wafanyakazi kitaifa inafanyika mkoani Iringa na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Magufuli na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi za jamii kulenge kuimarisha maslahi ya wafanyakazi“.
Chanzo : Nipashe
Post A Comment: