Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amewaita wanafiki wale wote wanao jadili penati yao waliyo pata dhidi ya timu ya Tanzania Prisons ambayo ilipigwa na mshambuliaji, Emmanuel Okwi na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa mabao 2 – 0.
Manara kupitikia kipindi cha michezo cha radio Magic FM amesema kuwa wanao jadili penati hiyo hawana haki ya kufanya hivyo kwa maswala ya Simba SC kwakuwa hata mchezaji wa hasimu wao Yanga SC,  Kelvin Patrick Yondan alivyoshika mpira dhidi yao hawakusema chochote.

Hawa wanao jadili hawana haki yoyote ya kujadili maswala ya Simba SC, wakati mchezaji wa Yanga SC, Yondani alivyoshika hawakusema chochote kwa hiyo ni unafiki tu hamna jambo lingine lolote.
Wakati penati ya wazi waliyoshika hakuna yoyote aliyesema katika hao huu unaitwa unafiki, hiyo penati wanayo isema mbona Yondani aloivyoshika haku aliye sema wala kuandika chochote kwenye mitandao yao, haya tufanye ile penati siyo tumepata goli 1- 0 hizo pointi tatu tumepata hatuja pata ni unafiki tu mimi simtaki mtu mnafiki namueleza waziwazi kuwa huo ni unafiki.
Tulipata penati ya wazi na Yanga SC nchi nzima iliona hakuna yoyote aliyeenua mdomo wake na kusema haya tufanye hiyo tuliyopata imefutwa alafu tuone kama hizo pointi tatu tumepata hatuja pata unafiki tu na kupoteza heshima yao katika jamii.
Yoyote aliyesema penati tuliyopata siyo sahihi ni wanafiki wao wanategemea Simba SC ifungwe na haifungwi ng’o.
Simba SC sasa hajafungwa hata mchezo mmoja toka kuanza kwa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu huu huku ikiwa na jumla ya pointi 58, wakati wanao shika nafasi ya pili Yanga SC akiwa na 47 na michezo miwili mkononi na nafasi ya tatu ikiwa timu ya Azam FC wenye alama 46
Share To:

msumbanews

Post A Comment: