Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limeeleza kuwa, baada ya kufanya mahojiano na msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, wamebaini kuwa vijana wengi hawana elimu juu ya sheria mpya ya mitandao iliyowekwa.

Akizungumza jana  Jumatano Aprili 18, Katibu wa BASATA, Godfrey Mngereza amesema kuwa baadhi ya watu wanaona kama msanii Diamond amelewa umaarufu jambo ambalo sivyo kama wanavodhani.

“Watu wanaweza kuchukulia hiyo kwamba Diamond amelewa umaarufu, amelewa mafanikio. Lakini mimi niseme kama baraza na masimamizi wa wasanii wote, tusimhukumu mtu kabla hatujamsikiliza wala kuongea nae. Sidhani kama ni umaarufu uliompelekea Diamond kufanya mambo kama hayo,” ameema Mngereza.

Mngereza amesema sababu kubwa ya wasanii na vijana wengi kufanya makosa ya kimtandao ni kutokana na sheria hiyo kuwa mpya kwao na hivyo kutaka elimu ya kutosha juu ya sheria hiyo kutolewa ili iweze kueleweka na kufuatwa.

“Kwa vijana wengi wa kitanzania ni sheria mpya. Tunahitaji kuwaelimisha zaidi kwamba kuweka picha au clip za aina hii hazikuongezei umaarufu,” amesema.

hatua hii imekuja ikiwa ni siku chache baada ya msanii Diamond kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano, baada ya kuweka katika mtandao wa instagram video zinazomuonyesha akiwa katika faragha na mama watoto wake, Hamisa Mobeto.

Hatua hiyo iliibua maswali mengi kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wa muziki wake, kwani tukio hilo limetokea siku chahe baada ya kuvuja kwa video iliyowaonyesha msanii Nandy na Bilnass nao wakiwa katika faragha.

Jambo hili liliwafanya watu wengi kuibuka na mwaswali, huku wengine wakidhani ni ‘kiki’ ambayo ingefuatiwa na kuachiliwa kwa wimbo ama video mpya kutoka kwa wasanii hao.

Hata hivyo, wasanii hao wote, Diamond, Nandy, Bilnass pamoja na mwanamitindo Hamisa Mobetto walishikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano yaliyochukua muda wa saa kadhaa, kisha kuachiliwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: