Serikali imeunda timu ya kufanya mapitio katika viwanda vya serikali vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi, ili virejeshwe serikalini.

Hayo yamesemwa jana Aprili 19, 2018 Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kipindi cha maswali na majibu ya hapo kwa papo.

“Serikali imeunda timu ya kufanya mapitio kwenye viwanda vyote vya serikali vilivyo binafsishwa ambavyo havifanyi kazi ili virejeshwe serikalini,” alisema na kuongeza.

“Viwanda vyote vilivyobinafsishwa vitarejeshwa serikalini na kutafutwa watu wengine ili viendelee kufanya kazi na kutoa ajira kwa watanzania.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: