Mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara inachezwa leo Uwanja wa Manungu mjini Morogoro kwa wenyeji Mtibwa Sugar wakiikaribisha Azam FC.
Tayari kikosi cha Azam kimeshawasili mjini Morogoro tangu jana kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 8 mchana.
Azam ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia pointi 46 huku ikiwa imecheza michezo 25.
Wakati huo Mtibwa Sugar yenyewe ina alama 33 ikiwa imecheza jumla ya michezo 24.
Post A Comment: