Baada ya klabu ya Simba SC Jumapili na jana kuibuka na ushindi wa goli moja bila dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, mashabiki wa timu ya Simba ambayo ipo katika mbio za ubingwa, wamekuwa wakituma mtandaoni vitu vya utani kwa mashabiki wa Simba.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda ambaye ni shabiki wa Simba, ametupia mtandaoni video inayomuonyesha msemaji wa Simba, Haji Manara akishangilia ushindi wa jana na kuandika ujumbe ambao umeonekana kuwaumiza mashabiki wa Yanga.
“Nasikia wana Yanga wanauliza lini tunaanza kuwapima tezi dume!,” aliandika RC Makonda kama kuwadhihaki mashabiki wa Yanga.
Wiki moja iliyopita mkuu huyo aliahidi kuanzisha kampeni ya upimaji wa tezi dume nyumba kwa nyumba ili kupuguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huyo
Post A Comment: