usherekea ushindi walioupata jana dhidi ya watani wao, Yanga SC, leo bungeni Dodoma Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ana taarifa za baadhi ya wabunge ambao ni wapenzi wa Yanga kutofika bungeni.
Akizungumza katika hali ya utani, Spika Ndugai amesema wabunge hao wameshindwa kufika kutokana kipigo cha hapo jana, huku akiwataja miongoni mwao ni Dkt. Mwigulu na Mkuchika.
Akizungumza katika hali ya utani, Spika Ndugai amesema wabunge hao wameshindwa kufika kutokana kipigo cha hapo jana, huku akiwataja miongoni mwao ni Dkt. Mwigulu na Mkuchika.
“Habari nilizonazo ni kwamba wabunge ambao wapenzi wa Yanga hawajaweza kufika Bungeni, naskia baadhi yao wamelala na viatu vitandani maana hawakukumbuka hata kuvua viatu,” amesema SpikaNdugai.
Hapo jana April 29 Simba SC waliibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Yanga SC, Simba walipata goli kupitia Erasto Nyoni dakika ya 37 kipindi cha kwanza
Post A Comment: