Ni ukweli usiopingika muigizaji Irene Uwoya na marehemu Agness ‘Masoganga’ Gerald walikuwa ni mashosti wakubwa – Tena kwenye shida na kwenye raha.
Kifo cha Masogange kimewaumiza wengi lakini Uwoya kimemgusa kwa ukaribu zaidi ukichana na familia ya marehemu. Irene kwa mara ya kwanza ameandika ujumbe tangu Masogange alipofariki dunia April 20 kwenye Hospital ya Mama Ngoma, Mwenge.
Irene Uwoya ameandika ujumbe huo mzito na wakusikitisha kwenye mtandao wake wa Instagram huku akionyesha hisia zake kali pamoja na pengo la moyoni mwake lililokuwepo baada ya kifo cha rafiki yake huyo kipenzi.
Kupitia mtandao huo Irene ameandika:
Siku zitapita na miaka itapita ila ntakukumbuka Milele kama rafiki wa kweli na mwenye mapenz ya dhati moyoni …najua ata ningetangulia mim ungefanya kama nilivyofanya…ntaendelea kukulilia kwa machoz ya ukimya …lakin pia kwatabasamu lahuzuni kwakuweza kutimiza Ndoto yako Japo hukufanikiwa kuiona…wewe ni mwanamke shujaaa!!!pumzika mama…I will always love u!!!
Post A Comment: