Video vixen Bongo, Tunda amedai yeye huwa hapigi picha za utupu bali watu wanavyomuona ndio mtindo wake wa maisha.

Tunda amesema picha za utupu ni pale mtu anapoenda studio na kupiga picha lakini zile anazopiga akiwa nyumbani kwake ni zinapaswa kueleweka ni picha za kawaida.

“Unajua kuna picha za utupu kwamba ile mtu unaenda studio unaamua kuwa wazi na kupiga picha, na kuna jinsi mtu anavyovaa kama ni nguo fupi yaani kawaida ya yeye kuvaa yapo si utupu kuna tofauti, mimi sipigi picha za utupu, no!,” amesema.

Tunda anametokea kwenye video za wasanii kama Young Dee, Chege na Temba na wengineo. Kwa sasa mrembo huyo katika mahusiano na mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: