Timu ya taifa ya vijana waliyo na umri chini ya miaka 17 ya Zanzibar, (Karume Boys) imetupwa nje ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge Cup U17 ) inayoendelea nchini Burundi baada ya kupeleka wachezaji waliyozidi umri.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye hapo jana siku ya Jumatatu ya Aprili 16 amekiambia chombo cha habari cha Xinhua kuwa walifikia maamuzi ya mwisho siku ya Jumapili baada ya kugundua Zanzibar ilikiuka sheria za mashindano kwa kusajili wachezaji wasiostahiki.
“Zanzibar imewakilisha wachezaji waliyozidi umri kwenye mchezo wa ufunguzi wa kundi B  dhidi ya Sudan siku ya Jumapili. Mchezo ambao haukuchezwa na ndipo tukagundua wachezaji wake 12 wamezaliwa kabla ya Januari 1 mwaka 2002, ambao wazi wamezidi umri unaotakiwa wa miaka 17,” amesema Musonye.
Timu ya Zanzibar imerudishwa nyumbani na kutakiwa kulipa faini ya Dola za Kimarekani 15,000 na kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kupeleka wachezaji waliozidi umri.
Musonye ameongeza kuwa ” Fedha hizo zitapelekwa kwenye Chama cha Mpira wa guu Kimataifa (IFA) ambao wao ndiyo wafadhili wa michuano hiyo ya CECAFA na kuitaka Zanzibar kutoshiriki michuano yote inayosimamiwa na Shirikisho hilo la Afrika Mashariki na Kati mpaka pale watakapo maliza kulipa faini.”
Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Somalia siku ya Jumapili timu ya Ethiopia imepigwa faini ya Dola 5,000 na CECAFA kwa kosa kama hilo huku wachezaji wake watatu wakitakiwa kurudishwa nchini kwao.
Kwaupande wandugu zao timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania Bara, (Serengeti Boys) ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mechi yake kwanza ya michuano hiyo siku ya Jumapili huku wenyeji Burundi ikipoteza kwa mabao 4 – 0 mbele ya Kenya mchezo uliyopigwa Jumamosi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: