Mara baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar hapo jana siku ya Jumatatu kwa jumla ya mabao  2 – 1,  Afisa habari wa klabu ya Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ‘Ligalambwike’ amesema kuwa hayo ni matokeo mabaya zaidi kwa upande wao na hivyo watajilaumu.

Kifaru amesema kuwa kupoteza mbele ya hasimu wao Kagera Sugar ni jambo la kujitaki “Mtibwa Sugar,  alitangulia kupata bao la mapema kupitia kwa Salum Ramadhan Kihimbwa na kabla ya mapumziko Kagera Sugar wakasawazisha na hivyo kumalizika kwa bao 1 -1 cha kipindi cha kwanza.”

Hata hivyo, Thobias Kifaru ameongeza “Kipindi cha pili kilikuwa cha mashambulizi kila upande ila Mtibwa tutajilaumu wenyewe kwakutokuwa  na umakini  katika sehemu ya ushambuliaji hasa yasehemu ya umaliziaji tulikuwa tukilifikia lango la Kagera Sugar  mara kwa mara,” amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar inatarajia kuondoka hii leo kuelekea Mwanza na kuweka kambi Shinyanga kwaajili ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United.
Matokeo ya michezo ya hapo jana siku ya Jumatatu Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: