Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi, limekiri kupokea rufaa ya Yanga yenye malalamiko mbalimbali ikiwemo suala la wachezaji wa Mbeya City kuzidi Uwanjani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amethibitisha kuwa rufaa hiyo kuwa tayari imeshawasili.
Wambura ameeleza kuwa wameishaipokea na sasa kitakachofuata ni kupelekwa ndani ya Kamati ya Masaa 72 kujadiliwa kisha watatoa mrejesho.
Yanga waliwasilisha rufaa yao ambayo tayari imeshalipiwa ikiwa ni saa kadhaa baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City kumalizika kwa sare ya 1-1 katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Post A Comment: