Mkuu
wa mkoa mstaafu Mzee Abbas Kandoro amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar alikolazwa kwa
matibabu.
Kabla ya kifo chake aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Singida na Mbeya na mikoa mingine.
Siku
mbili zilizopita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimtembelea na kumpa
pole Mkuu huyo wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambapo awali alikuwa
amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kabla ya
kuhamishiwa Muhimbili Dar ambapo umauti ndipo ulipomkuta.
Post A Comment: