Timu ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 17, Serengeti Boys imetwaa ubingwa wa CECAFA baada ya kuichapa Somalia kwa mabao 2-0 katika fainali iliyofanyika leo Aprili 29, 2018 mjini Bujumbura nchini Burundi.
Magoli ya Serengeti Boys yamefungwa na Edson Jeremiah na Jaffary Mtoo .
Kufuatia ubingwa huo, Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Milambo amesema ishara nzuri kwa timu ya taifa ya baadaye kwani itakuwa na vijana wazuri zaidi.
Serengeti Boys imetinga fainali baada ya kuifunga Kenya mabao 2-1 kwenye hatua ya nusu fainali huku Somalia wakiitwanga Uganda bao 1-0.
Uganda imechukua nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kenya goli 4-1 mchezo uliochezwa mapema kabla ya fainali.
Post A Comment: