Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita ilipitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 200 (Simba 2 vs Tanzania Prisons). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuwakilishwa na maofisa watatu badala ya wane kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 16, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kitendo chao ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 191 (Simba 3 vs Mbeya City 1). Klabu ya Simba imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika sita katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 12, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kitendo cha Simba ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo wakati adhabu dhidi yao imekijita katika Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Post A Comment: