Simba imezidi kuonesha kuwa ina kiu ya kuutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuilaza Tanzania Prisons kwa jumla ya mabao 2-0, mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa.

Simba walianza kupata bao la kwanza mnamo dakika ya 35 kupitia John Bocco aliyefunga kwa kichwa kufuatia krosi nzuri ya Erasto Nyoni aliyopiga na kugonga mwamba kisha mpira kumfikia Bocco ambaye bila ajizi akaukwamisha nyavuni.

Katika mchezo huo ambao Prisons walianza kucheza kwa kujihami, ulishuhudiwa dakika 45 za kwanza zikimalizika kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikipambana kucheka na nyavu, ambapo Simba walipata penati katika dakika ya 80 baada ya John Bocco kudondoshwa eneo la penati na ikatumiwa vema na mshambuliaji Emmanuel Okwi kuandika bao la pili.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 58 juu ya kilele huku ikifikisha idadi ya mabao 58 msimu huu, wakati huo watani zake wa jadi Yanga wakisalia na alama 47 kwenye nafasi ya pili.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: