Wakati Simba ikiingia kibaruani leo kuvaana na Lipuli FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara, inaelezwa wachezaji Emmanuel Okwi na Mlinda mlango, Aishi Manula wana kadi mbili za njano.
Uwepo wa kadi hizo mbili zitawafanya wachezaji hao kucheza kwa tahadhari kubwa kuhofia kuukosa mchezo dhidi ya watani wa jadi utakaopigwa Aprili 29 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kama Manula na Okwi watapata kadi nyingine za njano leo, tayari watakuwa wamekosa sifa ya kucheza dhidi ya Yanga, jambo ambalo linaweza kuzua hofu kwa Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre na mashabiki wa Simba kwa ujumla.
Simba itakuwa inawania alama tatu muhimu dhidi ya Lipuli iliyo Uwanja wake wa nyumbani, Samora, mjini Iringa.
Mchezo huo utaanza saa 10 kamili jioni na kurushwa mbashara na kituo cha Azam TV
Post A Comment: