Baada ya kuwasili kimyakimya jijini Dar es Salaam, kikosi cha Simba kinatarajia kuendelea na mazoei leo katika Uwanja wa Bocco Veterani.

Simba imewasili jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kambi yake ya wiki moja iliyokuwa imeweka mjini Morogoro kwa ajili ya kuiwinda Yanga katika mchezo wa ligi utakaopigwa Jumapili hii.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinaeleza hali ya wachezaji wote wapo sawa kiafya kuelekea mechi hiyo.

Kikosi hicho kinaenda kukabiliana na Yanga kikiwa juu ya msimamo wa ligi kwa kujikusanyia alama 59 dhidi ya 48 za Yanga.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: