BAADA ya juzi Jumatatu, Simba kushinda mabao 2-0 dhidi ya Prisons, timu hiyo imebakiza pointi 14 tu ili iweze kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kwa sasa Simba ina pointi 58, ambazo ni pointi 11 mbele zaidi ya Yanga inay­oshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kama Simba ikipata pointi 14 tu katika mechi zake sita za ligi kuu zilizobakia na kufikisha pointi 72, itakuwa bingwa kwani hazitafikiwa na timu yoyote ile.

Mechi za Simba zilizobaki ni dhidi ya Lipuli, Yanga, Ndanda, Singida United, Kagera Sugar na Majimaji.
Kocha wa Simba, Pierre Lechantre raia wa Ufaransa alisema atahakikisha kikosi chake hicho kinafikisha pointi 72 kwa kufanya vizuri katika mechi hizo zilizobaki.

Hata hivyo, alisema kuwa siyo kazi rahisi lakini atahak­ikisha wanazifikia mapema ili waweze kujitangazia ubingwa kabla ya ligi kumalizika.

“Ligi kwa sasa imefikia hatua ngumu, kila timu tutakayoku­tana nayo itakuwa inahitaji ush­indi ili iweze kuji­weka ka­tika nafasi nzuri kwenye msima­mo wa ligi kuu.

“Lakini tutahakiki­sha tuna­fanya vizuri ili tuweze ku­fikisha pointi hizo mapema na kujitangazia ub­ingwa,” alisema Lechantre
Share To:

msumbanews

Post A Comment: