Na George Mganga

Kesho ndiyo siku ambayo harusi ya Nyota wa Muziki Tanzania, Ali Kiba 'King Kiba' inatarajiwa kufanyika mjini Mombasa, Kenya, ambapo itarushwa mbashara na kituo cha Azam TV.

Inaelezwa kuwa shughuli za kisiasa mjini Mombasa zimesimama kwa muda kupisha tukio la harusi kufanyika ambapo Kiba atakuwa anafunga ndoa na mchumba wake, Amina Khaleef.

Tayari familia ya Kiba imeshawasili mjini humo wakiwemo washikaji zake, ndugu, jamaa na marafiki ambao wanasubiria tukio hilo kwa hamu kubwa.

Mbali na familia, uongozi wa Menejimenti yake ya Rockstar 4000 akiwemo Meneja Seven Mosha na Msanii aliye chini ya lebo hiyo ya Alikiba, Ommy Dimpoz, wote kwa ujumla wameshatia kambi Mombasa.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Tanzania, Jamhuri Kikwete, naye atakuwa mmoja wa wageni watakaohudhuria tukio hilo la harusi Alhamis ya kesho.

Harusi hiyo itafayika kwenye ukumbi mkubwa wa Diamond Jubilee uliopo mjini Mombasa ambapo viongozi mbalimbali kutoka NASA akiwemo Gavana wa jimbo hilo, Hassan Joho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: