Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shilole amefunguka kuhusu tuhuma za kuvujisha video ya utupu ya Nandy na Bill Nas, na kusema kwamba hahusiki na hajawahi kuona picha yoyote ya wawili hao wakiwa faragha.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Shilole amesema post aliyoweka insta kuhusu kuwa na picha za faragha za wawili hao alikuwa anatania, lakini ukweli ni kwamba hana picha yoyote na hajawahi kuona picha yoyote kabla.
Akiendelea kutoa utetezi wake Shilole amesema hahusiki kwenye kuvujisha video hiyo, isipokuwa inawezekana kuna mtu alikuwa nayo akapata kisingizio baada ya Shilole kupost ili aonekane ni yeye aliyevujisha.
“Hamna kitu kama hicho, mimi nilileta mzaha na nilitania tu, ni kama vile unamwambia mtu tuone kama kesho utaamka, kesho mtu anakufa kweli unaonekana ndiye wewe, kumbe watu walikuwa na mambo yao tayari, lakini kiukweli sihusiki, sijawahi kuziona nimetania, hiyo ni mtu ametembea na link au mtu alikuwa anatafutia sababu”, amesema Shilole.
Hivi karibuni baada ya video ya utupu ya Nandy na Bill Nas kuvuja mtandaoni, watu wengi wamekuwa wakimtuhumu Shilole wakiamini ndiye kavujisha, baada ya kusema kwamba ana picha nyingi za faragha za wawili hao, kwenye ukurasa wake wa instagram.
Post A Comment: