Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonyeshwa kukerwa na utamaduni wa baadhi ya vijana kupendelea kutumia lugha ya matusi mtandaoni.
Muigizaji huyo amesema badala ya vijana kufanya hivyo ni vema wakatafuta nafasi za kubadilisha maisha yao kwani bado zipo, pia kuacha kutumia muda mwingi kufanya vitu ambavyo havina faida na maisha yao.
Muigizaji huyo amesema badala ya vijana kufanya hivyo ni vema wakatafuta nafasi za kubadilisha maisha yao kwani bado zipo, pia kuacha kutumia muda mwingi kufanya vitu ambavyo havina faida na maisha yao.
“Tusiishi kwa kudharauliana, kutukanana, kujiona wewe bora kuliko mwingine, hizi team pia za mitandaoni ziache kutukana jamanii. Utajisikiaje unitukane leo kwenye page yako halafu kesho nife mbele yako uje uandike R.I.P?,” amesema Shamsa.
“Tutumie mitandao yetu vizuri, mbele ya Mwenyezi Mungu hakuna star, tajiri, masikini, kilema, mzuri, mbaya,..Inshaallah Mwenyezi Mungu atupe mwisho mwema,” amesisitiza.
Kwa sasa katika tasnia ya burudani Bongo kumetanda wigu jeusi kufuatia kifo cha aliyekuwa video vixen na muigizaji, Agness Gerald ‘Masogange’ ambaye alifariki jana April 20, 2018.
Mara kadhaa Shamsa Ford amekuwa akitoa nasaha mbali mbali kwa vijana. Hivi karibuni katika mahojiano na Bongo5 alisema hakuna mwanaume anayeweza kumfanya mwanamke chombo cha starehe ila inategemea mwanameke husika anajiweka vipi.
“Mwanaume hawezi akakufanya chombo cha starehe inategemea wewe na akili yako, kama unataka kuchezewa?, utachezewa basi, kama unataka uwe mwanamke wa maisha yake utakuwa kwa hiyo inategemea,” Shamsa Ford
Post A Comment: