Serikali imesema inaridhishwa na mwenendo wa utoaji wa elimu katika shule za sekondari za Kata na kusema bado itaendelea kuzijengea uwezo kwa kuboresha miundombinu ya shule hizo.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Kakunda na kusema hadi kufikia Oktoba mwaka jana kulikuwa na shule za kata zaidi ya 3,103 zilizokuwa na wanafunzi 197,663.

Aidha amesem a kupitia tafiti zilizo fanywa kuhusu elimu, serikali bado inaendelea na ujenzi wa shule mpya, ujenzi wa madarasa, vyoo, maabara, mabweni, nyumba za walimu ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vitabu vya ziada na kiada.

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Mheshimiwa HAMID BOBAL aliyetaka kujua tathimini iliyofanywa na serikali juu ya ubora na matatizo yaliyopo katika shule za sekondari za kata
Share To:

msumbanews

Post A Comment: