Majadiliano yanaendelea kati ya serikali na wamiliki wa shule binafsi kuangalia namna gani ya kutoza ada ambazo zitaakisi maisha ya Watanzania.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ameeleza hayo leo bungeni Dodoma leo wakati akijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliyetaka kujua kwa nini serikali isiwaachie wamiliki hao wa shule wajipangie ada na kuweka viwango vya madaraja ya ufaulu.
Naibu Waziri amesema, serikali haiwezi kuwapangia kiasi cha ada wala kuingilia maamuzi yao ila akabainisha kuwa majadiliano yanaendelea baina ya pande hizo mbili kuona namna gani ya kuweka gharama zinazoakisi hali halisi.
Akizungumzia suala la shule kujiwekea viwango vya ufaulu, Ole Nasha amesema udhibiti wa viwango vya ufaulu ni suala la kisera hivyo serikali haiwezi kuwaacha wamiliki wajiamulie bila kufuata sheria na taratibu.
“Kuna wanafunzi wamefukuzwa bila kufuata taratibu…wengine wamefukuzwa wakiwa kidato cha nne,” amesema Naibu Waziri huku na kusisitiza suala la utaratibu kufuatwa.
Akiuliza swali la msingi kwa niaba ya Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga, Selasini alitaka kufahamu ikiwa serikali haioni umuhimu wa wa kuondoa baadhi ya kodi zisizo na tija ambazo zimekuwa kero na kutoa ruzuku kwa shule hizo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: