Semina kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi imetolewa kwa waandishi wa habari mkoani Arusha  kwani wao ndio nguzo kubwa ya kuunganisha wataalamu wa afya na jamii lengo likiwa ni kuelimisha jamii.

Akizungumza na Msumba news Blog mganga mkuu Arusha Dkt.Onanji Vivian amesema kuwa wamefanya semina hiyo kwa waandishi wa habari  kwa sababu itakuwa rahisi kwa jamii kupata elimu hii ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Hata hivyo ameendelea kusema kuwa wao kama timu ya uwezeshaji wa huduma za afya  mkoa wa Arusha na wataalamu wa afya duniani WHO wamefanya semina hiyo kwa waandishi wa habari ili taarifa watakazoziandika na uhamasishaji watakaoufanya ukawe na ukweli ndani yake ili jamii ifahamu kuwa chanjo hii ni salama.

Aidha amesema kuwa chanjo hii itatolewa kwa watoto wenye miaka kumi na nne na zoezi hilo litazinduliwa rasmi tarehe 25/4/2018.

Kwa upande wake daktari mwandamizi tamisemi Dkt.Bonifas Nguvun amesema kuwa chanjo hiyo itatolewa kwa watoto kwanzia miaka tisa mpaka kumi na nne kwani chanjo hii hailengi walioanza kujamiiana badala yake inawalenga wale ambao hawajawahi kujamiiana.

Pia ameongeza kuwa chanjo hii haitahusika kwa watu wazima kwani haitoweza kufanya kazi ipasavyo na kusema kuwa inapaswa mtu kupata chanjo kabla ya kuanza kujamiiana.

Nae Bi Vero Mheta ambae ni mwandishi wa habari amesema kuwa wanahabari wako tayari kutoa elimu kwa jamii kuhusu chanjo hii lakini pia ametoa wito kwa wasichana wenye umri wa miaka tisa mpaka kumi na nne kujitokeza kupata chanjo hiyo kwani ugonjwa huo umepoteza wasichana wengi na hata vijana
Share To:

msumbanews

Post A Comment: