Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea tena usiku wa leo ambapo mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich watakuwa wanaikaribisha Real Madrid.

Real Madrid tayari wameshatua mjini Bayern ambapo nguvu zao kubwa wameziweka kwenye mashindano hayo hivi sasa.

Madrid haina nafasi tena katika taji la La Liga kutokana na ubora wa mpinzani wake, FC. Barcelona ambaye ameshajiwekea mazingira mazuri ya kutwaa Kombe hilo huku akitupwa nje ya UEFA Champions League na AS Roma.

Nyota Cristiano Ronaldo anapewa nafasi ya kuendelea kucheka na nyavu kwenye mashindano haya ambapo mpaka sas anaongoza kwa kuwa na mabao mengi.

Ronaldo atakuwa anamuwakilisha Messi kutokana na ushiriki wa Madrid ambayo inacheza La Liga pia nchini Spain leo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: