Wakati tasnia ya burudani Bongo ikiendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, msanii wa muziki wa hip hop, Roma ametoa ushauri kwa waombolezaji kuhusu picha zinazosambaa kwa kasi mtandaoni za mrembo huyo.
Roma ameeleza wakati watu wakiendelea kuomboleza kifo cha mrembo huyo ni vema wakatumia picha zake zenye staha tofauti na ambazo zimekuwa zikitumika na baadhi ya watu. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Roma ameandika;
“Wazo langu, ni vema tuonyeshe hisia zetu kwa kupost picha zake zenye staha, ili tumpunguzie adhabu ya kaburi,” amesema Roma.
Roma ameendelea na kuongeza kuwa, “A soldier Die, A soldier Born, Chill Easy Baby, Aggy Gerry,”.
Agness alipata umaarufu mkubwa pindi alipotokea katika video ya msanii Belle 9 ambayo ilikwenda kwa jina la Masongange ndipo na yeye kuanza kutumia jina hilo. Masogange amefariki jana April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

Post A Comment: