Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
IKIWA  leo ni siku ya 15 tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda atangaze kuwasaidia watoto waliotelekezwa na baba zao, hatimaye watoto 2,971 wamepatiwa bima za matibabu ya afya bure, baada ya wazazi wao kutopatikana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa mbali na kuwakatia bima ya afya watoto hao, lakini pia wamesikiliza zaidi ya kesi 7,184, ambazo  zinadhihirisha wazi kuwa katika mkoa huo kuna matatizo mengi tofauti na jamii inavyofahamu.

Mkuu huyo wa mkoa amesema, “Kutokana na zoezi hili tumebaini kuwa sio kina mama tu waliotelekezewa watoto na waume zao, bali hata kina baba wasiopungua 200 waliripoti ofisini kwangu kwa madai ya kutelekezwa na kuachiwa watoto na wake zao.”
Kwakugundua tatizo hilo Makonda ameandaa timu ya wataalamu wasiopungua 15, ambapo watatu wanatoka katika dawati la jinsia, watatu ustawi wa jamii, asasi zinazopigania haki za watoto na wanasheria wabobezi, ambapo jopo hilo linatarajiwa kufanya kazi kuanzia Mei 5 mwaka huu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: