Mkuu wa Dar es salaam, Paul Makonda ameziomba Mamlaka za Elimu kufunga shule kwa siku mbili kufuatia mvua zinazoendelea katika jiji hilo.
RC Makonda ameyasema hayo leo wakati akikagua maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Dar es salaam.
“Nimeziona Mamlaka za elimu kufunga shule kwa siku mbili, hadi tutakapowaambia siku ya Jumatano kulingana na hali itakavyokuwa kwasababu mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi yamejaa mengi kwa hali hii sio salama,” amesema RC Makonda.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa akiongea na Mwandishi wetu amethibitisha taarifa hizo ambapo amesema kuwa watu sita wameripotiwa kufariki katika wilaya za Kinondoni na Ilala huku mmoja akiripotiwa kufariki katika wilaya ya Temeke.
Post A Comment: