Rais John  Magufuli amewaonya viongozi wenye migogoro hususani wilayani Kondoa, kuacha kutofautiana na wakae pamoja ili kuyamaliza matatizo yao na kusisitiza pande zote zenye migogoro kuanza upya na kwamba siyo kila tatizo lazima lifikishwe kwake.

Rais Magufuli amefunguka hayo leo Ijumaa  mjini Kondoa wakati wa ufunguzi wa barabara ya Dodoma hadi Babati yenye urefu wa kilomita 251.

Amesema, Tanzania ni moja na watu wote wanahitaji maendeleo hivyo migogoro ya baadhi ya vingozi inachelewesha maendeleo ya wananchi.

"Viongozi wa Kondoa muache kugomba leo nimeona niwape meseji live muache kugombana niliwateua mimi nitawatoa mimi. Kuna wakati unakuta Hanang na Kondoa wanagombania mipaka utafikiria ni nchi jirani hilo nalo linakaa muda mrefu hata viongozi wanashindwa kulitatua hivyo ifike mahali tumalize migogoro hii" Rais Magufuli.

Ameongeza "Siyo kila mgogoro, lazima uletwe kwa rais. Nitaimaliza mingapi?  Viongozi waliopo washughulikie migogoro ya saizi yao. Tanzania ni kubwa na inachangamoto nyingi, hivyo ninyi ni viongozi mnatakiwa muelewane kwa manufaa ya wananchi wenu.  Nafahamu viongozi hampendi kuzungumzwa hadharani. Mimi nazungumzaga tu ndiyo tatizo langu. Naomba mkaniombee labda nibadilike," amesema rais Magufuli.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: