Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameshinda tuzo ya The African Prestigious Awards 2017 kwenye kipengele cha kiongozi bora wa bara la Afrika.

Tuzo hizo ambazo zimetolewa Aprili 15, 2018 Wikiendi iliyopita jijini Accra nchini Ghana pia zilishuhudia Watanzania wengine watatu katika tasnia ya filamu wakiibuka washindi.
Waigizaji hao ni Monalisa na Ray Kigosi waliyoibuka washindi kwenye vipengele vya Muigizaji bora wa kike barani Afrika na Muigizaji bora wa kiume barani Afrika.
Na mwingine ni mpiga picha Moiz Hussein ambaye ameshinda tuzo ya mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: