Rais John Magufuli amesimulia mara ya kwanza alipopelekwa mkoani humo kusoma kwamba hakula nyama kwa mwezi mmoja baada ya kutahadharishwa na watu kuwa akifika asile kitoweo hicho.

Akihutubia wakazi wa Iringa wakati wa ufunguzi wa barabara ya Iringa-Fufu jana Aprili 29, 2018; Rais Magufuli alisema alifika Iringa kwa mara ya kwanza mwaka 1978/79 kwa ajili ya masomo katika Sekondari ya Mkwawa.

“Niliambiwa usile nyama, usile mshikaki Iringa na kweli sikula," alisema na kwamba, baada ya kukaa muda alibaini wakazi wa Iringa hasa wanaume kuwa ni wakarimu.

"Wanaume wa Iringa ni wapole sana, unamchokoza lakini anajinyonga yeye badala ya kukuadhibu wewe," aliongeza Rais Magufuli huku akishangiliwa na umati wa wananchi.

Anasema watu wa Iringa ni tofauti na wenzao wa mkoani Mara ambao ukiwachokoza utakiona cha mtema kuni
Share To:

msumbanews

Post A Comment: