Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof J’
MKONGWE kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof J’, amefunguka kuwa yupo mbioni kumtembelea muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambaye yupo Gereza la Segerea.
Elizabeth Michael ‘Lulu’
 Akipiga stori na Star Showbiz, Prof J anayebamba na Ngoma ya Pagamisa alisema kama msanii na mdau wa sanaa Bongo, anatafuta nafasi siku moja aweze kwenda kuonana naye.

“Ninatamani kuonana na Lulu na niweze kuzungumza naye. Ninafahamu ana mengi ya kuzungumza, kwa hiyo ninapanga muda na ikiwezekana mtafahamu lini nitakwenda kuonana naye,” alisema Prof Jay.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: