Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo, April 17, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Prince William katika jumba la Kifalme la Buckingham Palace.

Katika mazungumzo yao Makamu wa Rais alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na imekuwa ikichukua hatua za kupambana na kuzuia ujangili ingawa teknolojia bado ni changamoto.
Kwa upande wake Prince Williams alimuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.
Pia Prince William amemwalika Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano unaohusu masuala ya Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu jijini London.
Makamu wa Rais Mhe. Samia yupo nchini Uingereza kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Madola.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: