Baada ya kufikia malengo yake ya mwaka 2017 kwa kufanya matamasha matatu makubwa nchini Ujerumani yaliyofana, Emanuel Austin ambaye ni mwalimu wa dansi (Choreographer) nchini humo ameanza mwaka 2018 kwa kitu kikubwa zaidi.
Austin ambaye ni mmiliki wa chuo cha dansi cha Tanzschule Weiss akishirikiana na mkewe Larissa Bertsch kilichopo katika mji wa Frankfurt, Jumamosi ya April 21 waliandaa tamasha kubwa ambalo lilijaza nyomi ya watu takribani 12,000.
Tamasha hilo limefanyika kwenye ukumbi wa Abschlussball. Akiongea na Bongo5, mwalimu huyo amesema tamasha hilo lilikuwa kali na lilifaana zaidi kitu ambacho kimeonyesha ni mwanzo mzuri kwao katika mwaka huu.
Post A Comment: