Usiku wa jana imefanyika sherehe nyingine ya harusi ya Alikiba na mkewe Aminah Rikesh Ahmed na mdogo wake Abdu Kiba na Ruwayda katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Sherehe hiyo ilifaana zaidi baada ya kuhudhuriwa na watu lukuki wakiwemo wazazi wa wana ndoa wote na watu maarufu pamoja na viongozi wa serikali akiwemo mke wa rais wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla na Gavana wa mji wa Mombosa, Hassan Joho ambaye pia ni mtu wa karibu wa msanii Kiba.
Mama Salma KKikwete (kushoto) akiwa na Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu
Katika sherehe hiyo Waziri Kigwangala amewataka maharusi wote kuchagua sehemu yoyote ya kitalii ndani ya Tanzania kwenda kufanyia fungate yao na yeye atagharamia kila kitu.
Waziri Kigwangalla akitoa neno kwa maharusi
Mama mzazi wa mke wa Alikiba (Aminah Rikesh Ahmed)
Post A Comment: