Unaikumbuka #Pogback? Hashtag maarufu sana Twitter wakati Paul Pogba akinunuliwa kwa dau la £89m kwenda United, Manchester walionesha umwamba wao wa pesa na dunia nzima ikajua kweli United wanataka kurudi juu.
Msimu wa kwanza EPL kwa Mfaransa huyu ukawa mgumu mno, maneno yakaanza. Wakasema Paul Pogba apewe msimu mwingine EPL ili azoee ligi hiyo kwa mara nyingine na msimu wenyewe ni huu.
Achilia mbali kiwango kikubwa ambacho alikionesha katika Manchester Derby, lakini msimu huu Paul asilimia kubwa ya vitu alivyoonesha ni rangi za nywele, mitindo ya kusalimiana na kushangilia.
Mwezi January Paul Pogba aliingia kwenye mzozo ambao haukuonekana mkubwa lakini inaonekana kama tatizo kwa Mourinho, hii ni baada ya majibizano katika mstari wa kuingilia uwanja wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham.
Tangu January baada ya tukio hilo, United walicheza takribani michezo 12 na kati ya hiyo kuna michezo 7 ambayo baadhi alitolewa, mingine hakucheza kabisa na mingine aliingia kama sub, na hii ina maana michezo 5 pekee ndio alicheza yote.
Pogba ameshalia na Mourinho kuhusu nafasi anayochezeshwa akidai uhuru zaidi uwanjani, na wakati Kelvin De Bryune akiwa ametengeneza nafasi 103 katika EPL, Pogba ametengeneza nafasi 34 tu na yuko nafasi ya 31 katika watengeneza nafasi.
Hata katika wachezaji ambao wamepiga pasi nyingi zilizowafikia walengwa bado Pogba anaonekana kuyumba, amepiga pasi 1435 huku akiwa nafasi ya 18 na Granit Xhaka anayeongoza orodha ya wapiga pasi timilifu ana pasi 2711.
Katika mchezo dhidi ya West Bromich wiki iliyopita, Paul Pogba aligusa mpira mara 75 na katika mara zote hizo hakuna hata mara moja aliyogusa mpira katika box la wapinzani na hii inamuweka kitimoto zaidi.
Kuna habari kwamba Jose Mourinho hana mpango na wachezaji walioboronga dhidi ya West Brom, hana mpango wa kuwapanga dhidi ya Tottenham na inadaiwa kwamba wengi ndio wataondoka.
Mourinho ameanza kuwaza kumpunguza Paul Pogba katika kikosi chake, na habari ni kwamba ni kati ya wachezaji ambao watawekwa sokoni dirisha lijalo la usajili, Mou ndio boss United na ndio anataka timu yake iweje kama amemchoka Pogba baasi ni wazi anakaribia kuuzwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: